Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu.
Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na
kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.
"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"
"endelea"
"bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba
shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka
polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua.
Yesu atanisamehe?"
"utasamehewa"
"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya
nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili
peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"
"utasamehewa"
"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa
kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi, nikaona
ananiwekea kiwingu, Kutazama huku na huku nikagundua tuko
wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"
"utasamehewa"
"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati
napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza
mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta
yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake
inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa.
Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu
kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua
tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto.
Yesu atanisamehe na hilo?"
-
kimya........
"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"
- kimya.........
Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye
kona moja akaona kabati la nguo za mapadri kama
linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya
majoho anatetemeka.
"sasa baba mbona umenikimbia?"
padri kwa taabu akajibu "nilitazama huku na huku nikagundua
kuwa tuko wawili peke yetu........"